Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawekezaji wa viwanda vya simu janja wakaribishwa nchini

Smartphone 636x489 Nape amezungumza na wawekezaji toka Canada

Fri, 27 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewakaribisha wawekezaji kutoka Canada kuja kuwekeza katika viwanda vya utengenezaji wa simu janja hapa nchini.

Nape amesema hayo katika kikao cha kubadilishana uzoefu na Katibu wa Mambo ya Nje wa Canada, Robert Oliphant ambapo walijadili masuala mbalimbali ya habari na teknolojia ya habari, katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam.

"Eneo ambalo tulitamani kama serikali kupata wawekezaji, ni eneo la upatikanaji wa simu janja (smart phones na tablets), ili ziwe bei nafuu na watu waweze kumudu kununua," alifafanua Nape.

Aliendelea kusema kuwa, kutokana na Tanzania kutokuwa na viwanda vya kutengeneza simu janja imesababisha vifaa hivyo kuwa na gharama ya juu, hivyo kupelekea idadi chache ya Watanzania kuweza kumiliki simu hizo.

Nape amesema kuwa, ni asilimia 27% tu ya Watanzania ndio wanaomiliki simu janja na asilimia inayobaki wanamiliki simu za kawaida, kutokana na gharama ya simu janja kuwa ya juu.

"Sasa imefika wakati simu janja zizalishwe hapa nchini, ili bei iwe ya chini na kila Mtanzania aweze kupata kifaa hicho, na hata huduma ikiboreshwa ina maana watu wengi watapata hiyo huduma," alifafanua Nape.

Kwa upande wake, Katibu wa Mambo ya Nje wa Canada, Robert Oliphant amesema kuwa ili Tanzania iweze kuwa na mawasiliano ya uhakika inatakiwa kuweka vipaumbele eneo la nishati, maendeleo pamoja na watu wenye ujuzi wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live