WAWEKEZAJI wa ndani wameiomba Serikali kuwapa kipaumbele na kuwawekea mazingira wezeshi huku ikiweka tozo kubwa kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi, ili kuviimarisha viwanda vya ndani.
Ombi limetolewa leo na wawekezaji wa viwanda vya kuzalisha vipodozi na mafuta, wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa, ya kutembelea viwanda hivyo ili kusiliza changamoto zinazowakabili.
Wamesema licha ya bidhaa wanazozalisha kuwa na soko, bado wanakabiliana na ushindani mkubwa kutokana na uwepo wa bidhaa kutoka nje ya nchi, ambazo nyingine uzalishaji wake hauna ubora.
Aidha, DC Mgandilwa amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto zinazowakabili wawekezaji, ili kuwasaidia kufanya shughuli zao vizuri.
Ameongeza kuwa lengo la ziara yake ni kuona namna ambavyo Serikali inaendelea kujenga mahusiano mazuri na wenye viwanda lakini, na kushirikiana nao katika miradi ya kijamii.