Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawekezaji sekta ya madini wakaribishwa Mbeya

Madini Pic Data Wawekezaji sekta ya madini wakaribishwa Mbeya

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema serikali imeendelea kuweka mazingira nafuu kwa wawekezaji katika sekta ya madini mkoani humo ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Homera ameyasema hayo alipofanya mahojiano kwenye Kipindi cha Jambo Tanzania na kusema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefuta leseni kubwa, ili kuwapa fursa wawekezaji wadogo hasa kwenye misitu ya Mbiwe na Itumbi kufanya uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Aidha Homera ameongeza kuwa asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na wenye ulemavu, kwa mkoa wa Mbeya kipaumbele kitakuwa kwa wale wanaojihusisha na uchimbaji wa madini.

''Tarehe 14 hadi 18 mwezi wa tatu tutakuwa na mambo mazito pale wilayani Chunya, mkoa wa Chunya wa madini''. amesema Homera na kuongeza kuwa "Mkoa wa Chunya wa madini unazalisha kilo 340 hadi 350 za madini kwa mwezi na serikali inapata zaidi ya bilioni 2".

Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa madini Tanzania baada ya mkoa wa Geita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live