Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawekezaji makaa ya mawe wapongeza bandari Mtwara

B0c56929b19631126d02c868481dac2c Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu ya bandari hiyo

Mon, 30 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawekezaji wa makaa ya mawe nchini, wameeleza kufurahishwa na serikali kwa kuboresha Bandari ya Mtwara, ambayo kwa sasa inawawezesha kusafirisha bidhaa hizo kwenda sehemu mbalimbali duniani kwa urahisi.

Meneja wa usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka kampuni ya Ruvuma Coal Limited, tawi la Bandari, Saidi Gadafi amesema Bandari ya Mtwara kwa sasa ina vifaa bora na vya kutosha, ambavyo vinawawezesha wawekezaji hao kusafirisha bidhaa zao kwenda masoko mbalimbali duniani.

"Kwa uwekezaji ambao serikali imefanya tumeona faida yake kwa sababu tulikuwa na programu ya meli moja kila baada ya miezi mitatu, lakini kutokana na facilities ambazo Bandari ya Mtwara inazo, imetuwezesha kuleta meli mbili na tuna uwezo wa kufanya meli tatu kwa mwezi," amesema.

Gadafi ameeleza hayo leo wakati wakipakia makaa ya mawe tani 59,660 kwenye meli ya Southern Cross katika Bandari ya Mtwara. Makaa hayo yanatarajiwa kusafirishwa kwenda nchini Uholanzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live