Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawekezaji NARCO wapewa mwezi kulipa deni la bilioni 6/-

7eb07a6cacea0e2b90534d5c6bdca421 Wawekezaji NARCO wapewa mwezi kulipa deni la bilioni 6/-

Thu, 14 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki ametoa mwezi mmoja kwa wawekezaji kulipa malimbikizo ya deni la Kampuni ya Ranchi za Taifa (Narco) ambalo ni zaidi ya Sh bilioni 6.

Waziri Ndaki ameutaka uongozi wa NARCO kufikia Februari 15 mwaka huu 2021, saba mchana awe amepata taarifa ya wawekezaji waliolipa madeni yao pamoja na ambao bado hawajalipa, kabla ya kuchukuliwa kwa hatua zaidi.

“Wawekezaji wote ambao tunawadai hapa Usangu na kwenye ranchi zingine wote walipe pesa ya NARCO tulipokubaliana kwenye mkataba tulikubaliana mtalipa pesa, mlipe madeni yenu ifikapo tarehe 15 mwezi februari saa saba mchana.” alisisitiza

“Tunataka NARCO ijiendeshe kibiashara, lakini sioni tukielekea kwenye kujiendesha kibiashara na moja ya matatizo yanayotufanya tusifike huko ni kulea watu wa namna hii.” amesema .

Amesema wale ambao hawatakuwa wamelipa hadi kufikia muda huo wanyang’anywe maeneo hayo ili wapatiwe watu wengine ambao wataweza kulipa kwa mujibu wa mkataba ili NARCO iweze kufikia malengo yake na kulalamika kuwa NARCO imechelewa kuchukua hatua kwa watu ambao wamekuwa na madeni ya siku nyingi.

Amesema kuwa wizara imefanya tathmini juu ya madeni hayo na kuagiza yalipwe katika viwango na tozo mpya zilizowekwa kwa sababu imejiridhisha kwamba kwa gharama hizo NARCO itaweza kujiendesha na kuhudumia vizuri ranchi zake.

Kwa mujibu wa taarifa ya NARCO iliyotolewa na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Masele Mipawa, maeneo ya vitalu katika ranchi za taifa yanayokodishwa kwa wawekezaji yamegawanywa katika viwango vitatu, ambapo kiwango cha chini ni Sh 3,500 kwa hekari moja kuanzia eneo lenye hekta 1 hadi 2000, kiwango cha kati ni Sh 5,500 kwa hekari moja kuanzia eneo lenye hekta kuanzia hekta 2001 hadi 5000 na kiwango cha juu ni Sh 7,500 kwa hekari moja kuanzia eneo lenye hekta zaidi ya 5001.

Chanzo: habarileo.co.tz