Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wawekezaji Czech na Poland wakaribishwa nchini

Rais Mwinyi Asifu Miaka 59 Ya Muungano .jpeg Wawekezaji Czech na Poland wakaribishwa nchini

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amekutana na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech na Poland na kugusia fursa zinazopatikana Tanzania hususani Zanzibar.

Fursa hizo ni pamoja na uchumi wa buluu, ujenzi wa hoteli, ujenzi wa viwanda, ushirikiano katika sekta ya elimu , umeme, sekta ya afya , miundombinu, kilimo na teknolojia ya uchumi wa kijani.

Rais Mwinyi amewakaribisha Tanzania Wawekezaji hao kutoka Jamhuri ya Czech na Poland ili waangalie fursa mbalimbali za uwekezaji na kibiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live