Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavuvi wapewa onyo matumizi ya baruti

Uvuvi Haramu Wavuvi wapewa onyo matumizi ya baruti

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wavuvi wilayani Kilwa mkoani Lindi wanaotumia baruti katika shughuli za uvuvi kuacha kufanya hivyo kwani wanajiumiza wenyewe.

Rais Samia amesema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa bandari ya uvuvi Kilwa Masoko.

Amesema matumizi ya baruti ndio yanayofanya wavuvi wafuate samaki maeneo ya mbali, kwani baruti zinahalibu matumbawe ya samaki na kusababisha samaki kukimbilia bahari kubwa.

"Kule mnapokwenda kama mnatumia baruti mjue mnajilipua wenyewe, mnalipua samaki lakini mnajilipua wenyewe, kwa sababu baadae hata huko bahari kubwa kutakuwa hamna samaki". amesema Rais Samia

Aidha, amewataka wasimamizi wa sekta ya uvuvi wilayani Kilwa kusimamia na kuwazuia wavuvi wasitumie baruti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live