Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wavuvi wachangia asilimia 1.8 Pato la Taifa

Wavuvi 780x470 Wavuvi wachangia asilimia 1.8 Pato la Taifa

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SEKTA ya Uvuvi kwa mwaka 2022 ilichangia asilimia 1.8 ya Pato la Taifa, huku ikikua kwa asilimia 1.9, Bunge limeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Baraza la Wawakilishi, Bakari Hamad Bakar, aliyetaka kujua kwa kiwango gani bahari zinachangia kukua kwa uchumi kupitia uvuvi.

“Sekta ya uvuvi hutoa mchango katika uchumi wa nchi, kupitia uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali zinazozalishwa ndani ya sekta.

“Aidha, baadhi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa hutumika kama malighafi katika uzalishaji ndani ya sekta nyingine kama vile viwanda na kuwa na mchango mkubwa zaidi katika sekta hizo.

“Katika mwaka 2022, sekta ya Uvuvi ilichangia asilimia 1.8 ya Pato la Taifa, huku ikikua kwa asilimia 1.9,” amesema Naibu Waziri.

Amesema katika mwaka 2022/2023, mazao ya uvuvi kutoka baharini yalichangia jumla ya tani 54,823.23 sawa na asilimia 10.68 ya mazao ya uvuvi ambayo ni tani 513,525.11.

“ Vilevile, maduhuli ya Serikali ya Shilingi Bilioni 1.8 yalikusanywa kutoka katika shughuli za uvuvi baharini. Kiasi hicho cha mazao ya uvuvi kilichozalishwa kutoka baharini kilitokana na uvuvi mdogo na kilikuwa na thamani ya Shilingi Bilioni 356.35,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live