Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wauzaji wa gesi majumbani lazima kuwa na mzani

Mtungi Wa Gesi Kutokuwa na mizani ni kosa kisheria

Fri, 20 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini imewataka wauzaji wa gesi za kupikia kuhakikisha wanakuwa na mizani za kupima gesi kwani kutokuwa na mizani ni kosa la kisheria.

Hayo yamesemwa na Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini Mhandisi Lorivii Long'idu wakati akitoa elimu kwa Wauzaji na wasambazaji wa gesi za kupikia majumbani semina iliyoandaliwa na kampuni ya taifa Gesi na kufanyika jijini Arusha.

Amesema kuwa ni kosa la kisheria wauzaji kuuza gesi bila kuwa na mizani hivyo wanapaswa kuhakikisha wanakuwa na mizani ili kuepuka hatua Kali za kisheria kwa wale watakaobainika kutokuwa na mizani hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live