Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wauza gesi watekeleza agizo la mizani

3a31e969b49274008ac69248420f0856 Wauza gesi watekeleza agizo la mizani

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asilimia 46 ya Wakala wa Kuuza Gesi wa Kampuni ya Manji (Manji's Gas) tayari wametekeleza agizo la Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (EWURA-CCC) la kila muuzaji kuwa na mizani kwa kununua mizani kwa ajili ya kupima uzito wa mitungi pamoja na gesi ndani yake.

Manjis Gas wameitikia agizo lililotolewa katika semina ya wadau na watumiaji wa gesi lililotolewa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Lorivii Long'ido jijini Arusha Mei 20, mwaka huu.

Meneja wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Manjis Gas katika Kanda ya Kaskazini na Kanda ya Kati, Kingsluga Francis akizungumza katika maonesho ya wakulima ya Nanenane mjini hapa, alisema wapo katika kampeni kuhakikisha kila wakala anayeuza gesi hiyo anakuwa na mzani wa kupimia.

"Kwa sasa asilimia 46 ya wakala wetu, wanaouza gesi yetu, wana mizani na tunaendelea na kampeni ili kuhakikisha wote wanakuwa na mizani," alisema.

"Tumekuwa tukifanya vikao katika kila kanda za Mbeya, Mwanza na Dodoma hii barabara ya tisa pamoja na Chamwino Ikulu tunahimiza wakala wetu kuwa na mizani ya kupima uzito wa mitungi na gesi ili kuwapa uhakika wateja wetu," alisema.

Francis alisema hata katika maeneo ambayo hakuna mizani wanawaelimisha wateja uzito unaojulikana wa mitungi na hivyo ukichanganya na uzito wa gesi lazima ijulikane jumla ni kilo ngapi.

Francis alisema kampuni yake imekuwa ikishiriki katika maonesho mbalimbali yaliyopita lakini katika maonesho ya mwaka huu, wameongeza bidhaa mbalimbali za kuonesha na kuuza zikiwemo jiko la kuchoma nyama kwa kutumia gesi.

Francis alisema pia kampuni yao imewaletea wananchi pia mashine bora ya kuongeza joto nje ya nyumba.

Pamoja na bidhaa hizo, katika maonesho hayo ya 28 ya Kanda ya Kati inayoshirikisha mikoa ya Dodoma na Singida, pia wameleta bidhaa za biashara na za matumizi ya ndani ya nyumba zikiwemo mashine za kutengeneza joto kwa wafugaji wa kuku hasa vifaranga.

Francis alitoa ushauri kwa watumiaji wa gesi majumbani au katika shughuli zao za kila siku kuchunguza mpira unaotumika kuunganisha gesi na jiko mara kwa mara kwani mara nyingi inaweza kuchakaa na kuleta athari za kuvuja na hivyo kuleta madhara katika nyumba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live