Kampuni ya Coca-cola kwanza imeanzisha kampeni maalumu ya kuwasaidia vijana 300 wanaofanya biashara ya chips wenye uwezo wa kuajiri wenzao watatu hivyo kukamilisha hesabu ya vijana 900.
Kampeni hiyo imelenga kutoa vifaa saidizi vya kufanyia kazi ikiwemo jiko la kisasa mtungi wa Gesi na vifaa vingine Ili kuhakikisha ufanisi unaongezeka katika biashara hiyo.
Akizindua kampeni hiyo meneja wa Masoko wa Coca-cola kwanza Victor Amosi amesema wamefanya utafiti na kubaini vijana wengi mkoa wa Dar es Salaam wamejiari katika kazi ndogo ndogo ikiwemo hii ya kuuza chips hivyo msaada huo utawasaidia wengi.
Kampeni hiyo pia imelenga kuwapa mafuzo vijana hao 300 watakaopatikana juu ya kutunza kumbukumbu zao na taarifa za kifedha sambamba na kupewa elimu ya matumizi ya matumizi ya majiko ya gesi ya kisasa.