Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watumishi mipakani waonya kuruhusu mifuko isiyokidhi viwango kuingia Tanzania

71806 Mifuko+pic

Fri, 16 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakurugenzi wakuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wamewataka watumishi wa Serikali ya Tanzania wa mipakani kufanya kazi kwa weledi ikiwamo kutoruhusu bidhaa zilizokidhi viwango kuingia nchini humo.

Wametoa kauli kwa pamoja leo, Ijumaa Agosti 16, 2019 wakati wakizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa biashara ya mifuko mbadala aina ya ‘Non – Woven’ ( kitambaa chepesi).

Wamesema kumekuwa na wimbi kubwa la mifuko hiyo isiyokidhi viwango vilivyowekwa na TBS kuingia Tanzania hali inayosababisha kuviua viwanda vya ndani vinavyozalisha mifuko hiyo.

"Mtumishi yeyote wa Serikali atakayeshirikia kuhujumu vita ya kupambana na mifuko ya plastiki,  mbadala isiyokidhi viwango yeye ni sawa na mhujumu uchumi," amesema Dk Samuel Gwamaka ambaye ni mkurugenzi wa NEMC

Mkurugenzi wa TBS, Dk Athuman Ngenya amewataka watumishi hao wa mipakani kuhakikisha mifuko ya non- woven inayoingia nchini inakuwa GSM isiyopungua 70 kama ilivyowekwa na shirika hilo na iwe nembo au jina la mzalishaji.

"Kwa wafanyakazi wa TBS wanayo taarifa ya wenzao wawili kusimamishwa kazi kule Arusha, hili suala ni endelevu. Ikigundulika umepitisha mifuko mbadala isiyokidhi  tutakuondoa na kukukabidhi kwa NEMC kwa hatua zaidi," amesema Dk Ngenya.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz