Tunduma. Watumiaji wa kituo cha forodha Tunduma kinachotoa huduma ya pamoja (One Stop Border Post-OSBP) kati ya Tanzania na Zambia, wamesifu uboreshaji huduma zinazotolewa.
Kituo hicho kilizinduliwa hivi karibuni na marais, John Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia.
Mmoja wa watumiaji wa mpaka huo, Zainab Jumanne anayeendesha lori la mafuta la kampuni ya Lake Oil, alisema toka mwaka 2009 amekuwa akipita mpakani hapo mara mbili kwa mwezi kupeleka mafuta Zambia, amekutana na changamoto nyingi kwa zaidi.
Zainab alisema uwapo wa foleni kabla ya ujenzi wa kituo hicho ulikuwa kero kubwa kwa watumiaji, ilikuwa ikifika saa 5:00 asubuhi madereva hawawezi kuvuka wanaegesha magari yao hadi siku nyingine kwa sababu wingi wa magari.
Hata hivyo, Zainab alisema ujenzi wa kituo hicho kipya cha forodha si tu kimepunguza au kuondoka usumbufu, bali kimeipa hadhi Tanzania.
Alisema zamani ilikuwa lazima upate huduma ofisi zote za mpaka wa Tanzania na Zambia, lakini hivi unapita upande mmoja na kuondoka.
Pia Soma
- Halmashauri Moshi yafungasha virago yahamia Kolila
- Hotuba ya Mwalimu Nyerere: Tuna kazi moja tu, kumpiga Idi Amin
- Chadema Jiji la Arusha yapata viongozi wapya
Alisema anafanya biashara kati ya Tanzania na Lubumbashi (DR-Congo), awali alikuwa akitumia muda mwingi kwenye foleni hali iliyokwa ikiwasababishia wafanyabiashara wengi kupoteza muda.
“Imekuwa rahisi sana hata kupata huduma za benki na Visa katika jengo hili lenye huduma za kimataifa,” alisema Musabududinda.
Mfanyabiashara wa viazi na kutoka Tunduma kwenda Nakonde Zambia, Daina Hussein alisema zamani walikuwa wanapita njia za panya siyo tu kukwepa foleni, bali kuogopa kutozwa ushuru.