Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu zaidi ya 6,500 wanavyokula kwenye mradi wa SGR

29025 Asg+pic TanzaniaWeb

Tue, 27 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kilosa. Wanasema “Asiyefanya kazi na asile” watu zaidi ya 6,500 wanakula kwenye mradi wa ujenzi mpya wa reli ya Standard Gauge (SGR).

Kuanzia mshika kibendera wa kuongozea magari hadi kwa mameneja wakuu wa uendeshaji wa mradi huo, madereva wa malori, mashine kama makatapila, buludoza zaidi ya 1,600 wako eneo la mradi kwenye awamu zote mbili.

Meneja wa mradi huo awamu ya kwanza kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, Machibya Masanja amesema wana mitambo zaidi ya 1,600 kwenye mradi mzima kuanzia Dar es Salaam hadi Dodoma ikiwa inafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika kama muda ulivyopangwa.

“Tuna malori, magari ya kawaida, makatapila, mashine za kushindilia, kuchimba udongo n azote hizo zinaendeshwa na watu hivyo unaweza kuona ni watu wengi kiasi gani wako kwenye ground wanafanya kazi,” amesema Masanja.

Katika mradi huo meneja mradi awamu ya pili wa kampuni ya Yapi Merkezi kuanzia Morogoro hadi Makutuporo Dodoma, Dk Husnu Uysal amesema wana wana waajiriwa wa ofisini wazawa asilimia 36.88 na wataalamu toka nje asilimia 63.12.

Anasema kwa upande wa wafanyakazi wasio wa ofisini waliopo kwenye ujenzi kuna asilimia 86.45 ya wazawa na wataalamu toka nje asilimia 13.55.

“Kwa ujumla tuna asilimia 72.68 ya wazawa kwenye mradi na asilimia 28.32 ya wataalamu kutoka nje hivyo ni sawa na kusema tuna wataalamu toka nje 291 kwenye mradi na wazawa 1,533 hiyo inafanya jumla ya wafanyakazi wote kuwa 1,924,” amesema.

Amesema wana mashine tofauti tofauti kama malori, makatapila na mengineyo kama 385 huku wakitegemea ziongezeke nyingine 220 ifikapo Desemba mwaka huu ili kwenda na kasi ya mradi ukamilike kwa muda uliopangwa.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz