Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu milioni 8 wanufaika na huduma ya minara nchini

Minara Mawasiliano Watu milioni 8 wanufaika na huduma ya minara nchini

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WATU zaidi ya milioni 8 wanatarajiwa kunufaika na minara 758 iliyojengwa na serikali mwaka jana licha ya changamoto zinazoikabili sekta ya mawasiliano ya simu nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye leo Mei 9, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa mjadala kuhusu sekta ya mawasiliano ya simu ulioandaliwa na Kituo cha Huduma ya Ushauri ya Mawasiliano ya Simu (LLC) cha nchini Marekani.

Aidha amezitaja changamoto zinazoikabili sekta hiyo kuwa ni pamoja na huduma za mawasiliano kuwa juu kutokana na gharama za uwekezaji huku akitolea mfano wa kuendesha mnara mmoja wa mawasiliano kwa mwezi kwa kutumia mafuta ya dizeli ni takriban Shilingi milioni 1.8 tofauti na kuunganisha mnara na umeme ambao gharama yake inafikia shilingi laki 4.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live