Boti ya chupa za plastiki ni moja ya kivutio kinachopatikana ndani ya Kisiwa cha Unguja, Zanzibar.
Boti hii, hutumika kuhifadhia taka za plastiki kama bilauri na chupa za maji, maalumu kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinazopelekea ongezeko la joto duniani.
Kituo cha Zanzibar ni kati ya vituo vitano vilivyo rodheshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuwa na kiasi cha juu cha ongezeko la joto nchini kwa mwaka 2023.
"Hadi kufikia Disemba 29, 2023 kituo cha Zanzibar kiliripoti nyuzi joto 33.4 °C mnamo tarehe 02 Disemba, 2023 (ongezeko la nyuzi joto 1.6)." Imeeleza taarifa ya TMA.