Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wateja kupata gawio la bil. 1/- Halopesa

Halotel Tanzania.png Wateja kupata gawio la bil. 1/- Halopesa

Tue, 2 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KWA mara ya kwanza Kampuni ya Mawasiliano ya Simu ya Halotel Tanzania italipa gawio lenye thamani ya shilingi bilioni moja kwa wateja wake wa Halopesa zaidi ya milioni 1.9 nchini kupitia huduma zake za kifedha za HaloPesa kuanzia mwezi huu wa Juni.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Biashara cha HaloPesa, Magesa Wandwi, alisema kuwa gawio hilo litalipwa kwa wateja binafsi, mawakala wa kusambaza huduma za HaloPesa na washirika wake ambao wanatumia huduma za HaloPesa.

“Wateja wa HaloPesa watapata gawio hili linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HaloPesa Trust, zilizoko katika benki mbalimbali nchini kati ya Oktoba 2016 na Desemba 2018,” alisema.

Alisema faida hiyo ni haki ya wateja na HaloPesa wanashauku kuwalipa wateja wao gawio hilo kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali toka Benki Kuu ya Tanzania.

“Gawio hili ni la kwanza kwa wateja wetu na litatolewa ndani ya mwezi mmoja toka sasa, kiasi cha gawio ambacho mteja wa HaloPesa atakipata anaweza kutumia atakavyo ikiwa ni pamoja na kutoa au kufanya miamala mbalimbali,” alisema.

Alisema Halotel inaendelea kutoa huduma bora zenye gharama nafuu nchi nzima na kuwaomba wateja waendelee kutumia huduma za Halopesa,

Pia, wamewakaribisha wateja wapya kutumia huduma za HaloPesa zenye huduma nafuu na pia kuwashukuru wadau wanaondelea kutumia huduma zao za HaloPesa.

“Tunaishuruku Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kutusimamia vizuri kwa sababu hizi ni pesa za wateja tunatimiza wajibu wetu wa kisheria na kanuni ili wateja wetu wanufaike,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live