Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wateja Twiga kuendelea kuhudumiwa na matawi yao

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya kuunganishwa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), wateja wa Twiga Bancrop wataendelea kupata huduma katika matawi yao kwa miezi mitatu ijayo wakati uunganishaji wa mifumo ukifanyika.

Taarifa hiyo ilitolewa jana ikiwa ni siku moja baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutangaza kuziunganisha benki hizo za Serikali, ili kuongeza ufanisi baada ya mtaji wa Twiga kutetereka.

Ofisa mtendaji mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi alisema baada ya kipindi hicho cha mpito, wateja wa Twiga wataanza kupata huduma katika matawi ya Benki ya Posta.

“TPB ina rekodi nzuri ya utendaji. Miaka sita iliyopita tumeongeza mtaji kutoka Sh8 bilioni mwaka 2010 hadi zaidi ya Sh60 bilioni,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz