Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania watakiwa kutojitumbukiza kwenye mikopo bila malengo

Pesa (3) Watanzania watakiwa kutojitumbukiza kwenye mikopo bila malengo

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watazania wameshauriwa kutopenda kujitumbukiza kwenye masuala ya mikopo kama hawajajipanga kwa kujua wanachotakiwa kukifanya.

Rai hiyo imetolewa juzi Februari 14, 2023 na  Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC), Dk. Beng’i Issa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Jijini Dodoma Juu ya utekelezaji wa Baraza hilo.

Mbali na kuwataka watanzania kutojitumbukiza katika mikopo ambayo hawajajiandaa nayo pia amewataka watanzania kuwa na nidhamu ya fedha sambamba na kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba yakita benki.

Akizungumzia ufanisi wa baraza hilo, Beng’i ameeleza kuwa kazi kubwa ni kuhakikisha wanawawezesha wananchi kupata fursa mbalimbali za kujikwamua kihuchumi.

Katika kutilia mkazo juu ya kuwawezesha wananchi ameeleza kuwa kwa sasa kuna mifuko mbalimbali ya kuwawezesha akina mama na vijana huku akieleza kuwa akina mama wamekuwa wakipewa kipaumbele zaidi kwa kuwa ni waaminifu katika kurejesha.

“Nataka kuwaeleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana baraza kwa kushirikiana na serikali kwa ujumla wake wametoa kiasi cha Sh. 5.6 trilioni kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wapatao milioni nane jambo ambalo ni hatua kubwa katika kuwawezesha watanzania kujiinua kiuchumi” ameeleza Beng’i. 

Sambamba na kutoa pesa hizo kwa ajili ya kuwawezesha watanzania milioni nane Beng’i amesema kuwa bado watanzania wengi wanakabiliwa na elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Kutokana na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha amesema kuwa serikali kwa kushirikiana taasisi mbalimbali kwa ajili ya kutoa elimu juu ya matumizi ya fedha na kumiliki fedha.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa watanzania ili kuhakikisha watanzania wanajikwamua katika maisha na kuishi maisha ambayo yatakuwa bora kila mmoja jambo ambalo litawafanya watanzania kuwa na amani na furaha,” amesema Beng’i.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live