Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa za Afcon 2027

Watanzania Watakiwa Kuchangamkia Fursa Za Afcon 2027 Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa za Afcon 2027

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimewasihi watanzania kuchangamkia fursa ya kuwekeza kwenye sekta mbalimbali kuelekea Mashindano ya AFCON 2027 Tanzania kuwa mwenyeji.

Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TIC, Gilead Teri Aprili 16,2024 jijini Dar es salaam kwenye Kongamano la Uwekezaji kati ya wadau wa sekta ya michezo, utalii na ukarimu kujadili fursa za uwekezaji kuelekea AFCON 2027.

Mkurugenzi huyo amesema, Watanzania wawekeze kwenye sekta ya madini, uchukuzi, migahawa, viwanda, mahoteli, pamoja na ujenzi wa viwanja vya michezo.

Ameongeza kuwa, kwa mwaka wageni milioni moja hadi mbili wanakuja kutembelea nchini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema, kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON 2027 yatakayoanza mwezi Juni, Tanzania imetoa zaidi ya Dola milioni 30 huku Kenya na Uganda nazo wakitoa Dola milioni 30 kwa kila mmoja jumla nchi zote tatu wametoa Dola zaidi ya milioni 90.

Amesema, Tanzania imejipanga kujenga na kukarabati viwanja vitatu kwa ajili ya mashindano hayo ikiwa ni Uwanja wa New Amaan complex wa Zanzibar, Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, na ujenzi wa Uwanja mpya wa Samia, jijini Arusha unaogharimu zaidi ya Sh bilioni 236.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live