Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wataja mafanikio uwezekezaji China- Tanzania

Chinatzbuiadf.png Watanzania wataja mafanikio uwezekezaji China- Tanzania

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wawekezaji kutoka China wakikutana na baadhi ya wawekezaji wa Tanzania, tayari fursa za ushirikiano zimeanza kuonekana.

Wawekezaji hao kutoka jimbo la Zhejiang (Jinhua) wamekuja wakati uwekezaji wa nchi hiyo ukiongezeka na kuifanya hiyo kuwa kinara cha uwekezaji mkuwa nchini.

Wakizungumza Septemba 25 katika mkutano huo, baadhi ya Watanzania waliohudhuria mkutano huo wamesema umekuwa wa mafanikio na tayari wameshaanza kunufaika na wawekezaji hao.

Miongoni mwao ni Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Baba Watoto linashughulika na maendeleo ya watoto na vijana kupitia kwenye Sanaa, Mgunga Mwa Mnyemelwa, aliyesema tayari wamepata mbia kutoka China.

“Tumeshiriki kongamano hili kwa nia ya kutafuta wabia na wadau wa kuendelea kushirikiana katika kuendeleza Sanaa na utamaduni.

Sasa tumepata tumepata mdau ambaye ni anaitwa Fashion Tourism Investment ya China inayotaka kuingia mkataba kufanya kazi na sisi, kwa hiyo hayo ni mafanikio,” amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Tanzania and China Friendship Promotion Association, Joseph Kahama amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio kwani umewaunganisha wawekezaji kutoka China na Tanzania.

“Sisi tuinapenda kuona Watanzania na Wachina wanendelea kuwa marafik, wakifahamiana katika tamaduni zao, biashara na mengine. Mtu ukifahamiana na mgeni mambo mengi yanaendelea,” amesema.

Mkurugenzi mtendaji wa Interbest Investment Co. Ltd, Augustine Masonga alisema kampuni yake inaagiza vifaa vya umeme kutoka China vinavyotumika katika umeme wa miradi ya Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA) na Tanesco.

“Kwa hiyo tunapoona wageni kama hawa kutoka China, inatusaidia kwa sababu tunajenga uhusiano kukuza biashara zetu,” amesema.

Naye Mhadhiri wa Jiografia, Utalii na huduma za Ukarimu, Celia Muyinga kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, amesema China ni soko kubwa la utalii kwa Tanzania.

Dk Celia aliyepata shahada yake ya uzamivu katika utalii nchini China, ameshauri Watanzania wanaoifahamu lugha ya Kichina kusaidia kuhamasisha watalii kutoka nchi hiyo.

“Tanzania tungekuwa na kanzidata ya watu waliosoma China ili wasaidie kufasirilugha kwa wageni kutoka nchi hiyo. Lugha isiwe kikwazo,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live