Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania washauriwa kununua vya nyumbani

Madein Tz Watanzania washauriwa kununua vya nyumbani

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

JAMII imetakiwa kununua bidhaa za samani zinazotengenezwa au kuuzwa na kampuni kutoka hapa nchini na kuacha kuagiza kutoka nje ya nchi ili kuunga mkono jitihada za kuendeleza bidhaa za ndani.

Wito huo umetolewa na Kaimu Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya GSM, Smart Deus wakati wa uzinduzi wa kampeni ya punguzo la bei la bidhaa zake ya “GSM home gulio extra 2021” .

Aidha alibainisha kuwa wapo watanzania wanaoagiza bidhaa moja kwa moja kutoka nje ya nchi na kukumbana na gharama kubwa wakati wanaweza kupata bidhaa hizo kutoka ndani ya nchi.

Alisema kwa kufanya hivyo wanakuwa wakipeleka nje ya nchi fedha nyingi ambazo zinaweza kutumika hapa nchini kwa kununua bidhaa za ndani.

Akizungumzia kuhusiana na kampeni yao hiyo alisema kuwa imelenga kutoa nafasi kwa wateja na wadau wake kufanya manunuzi samani mbalimbali katika msimu wa mwanzo wa mwaka.

Alisema imelenga kuwafikia wanunuzi wengi na kuimarisha mahusiano na wateja kwa kuweka bei nafuu.

“Mwaka 2021 utakuwa mwaka wenye neema kuleta bidhaa nyingi zenye ubora, bei nafuu na uhakika kwa watumiaji na siku si nyingi tumemaliza kampeni yetu ya kufunga mwaka na sasa tunawaletea Gulio Extra na wateja wetu watajizolea vitu mbalimbali kwa bei nafuu sana” alisema.

Alisema, kampeni hiyo iliyoanza jana itaisha Februari 28 mwaa huu huku ikihusisha maduka manne ya GSM home yanayopatikana Mikocheni, Dodoma Capital, Citty Mall, GSM Pugu na Mlimani City.

Chanzo: habarileo.co.tz