Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wahimizwa ufugaji nyukiWatanzania wahimizwa ufugaji nyuki

82444 Nyuki+pic Watanzania wahimizwa ufugaji nyukiWatanzania wahimizwa ufugaji nyuki

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya asali ya Tanzania kuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi, Watanzania wameshindwa kuitambua fursa zilizopo katika bidhaa hiyo.

Hali hiyo inatokana na wengi kutotambua ufugaji nyuki ni fursa pana inayoweza kuwa chanzo kikubwa cha kipato.

Hayo yameelezwa na kamishna wa uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania,  Profesa Dos Santos Silayo alipokuwa akizungumza na wanawake kutoka mikoa mbalimbali kupitia jukwaa la madirisha.

Jukwaa hilo linalenga kutengeneza vikundi vya wanawake wanaojihusisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kupitia viwanda vidogo.

Profesa Silayo amesema kuna fursa kubwa katika ufugaji wa nyuki, hasa soko la asali ambalo hadi sasa Tanzania imeshindwa kulikidhi.

“Asali ya Tanzania inasifika kwa ubora, kuna soko la tani 200,000 kwa mwaka nchini China lakini tunashindwa kukidhi mahitaji hayo kwa kuwa uzalishaji wetu ni mdogo.” “Tunazalisha chini ya tani 30,000 kwa mwaka ni kiwango kidogo, hili ndilo linalofanya Serikali iingilie kati kuhamasisha watu wengi waingie kwenye biashara hiyo,” amesema.

Amebainisha kuwa kupitia madirisha hayo ya wanawake wanaweza kufanya ufugaji huo na Serikali itakuwa tayari kuwawezesha katika namna mbalimbali ikiwemo kuwapatia mikopo.

“Kupitia mfuko wa misitu tumeanza kutoa mikopo kwa ajili ya wajasiriamali wanaojihusisha na ufugaji wa nyuki, ni kati ya Sh5milioni hadi Sh500 milioni, hivyo wanawake tumieni nafasi hii mkazalishe asali ya kutosha ili tukauze kwenye soko la kimataifa,” amesema Profesa Silayo

 

Chanzo: mwananchi.co.tz