Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watanzania wahaswa uzalendo ajira kwenye miradi nchini

WhatsApp Image 2021 04 19 At 19.14.29 (2).jpeg Watanzania wahaswa uzalendo ajira kwenye miradi nchini

Tue, 20 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella wakati alipotembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa awamu ya tano ( SGR LOT 5) Mwanza - Isaka amesema changamoto kubwa wanayoipata ni baadhi ya watu wanaopata fursa ya kufanya kazi kutokuwa waaminifu.

"Inabidi kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake nchi inakwenda kasi kwa sasa uzalendo,uaminifu  unahitajika sana na Rais wetu anasimamia miradi hii yote kwa ukaribu sana kwa sababu jambo ili lipo kwa maendeleo" amesema Mongella.





Naye Naibu Meneja Mradi huo Mhandisi Alex Bunzu, amesema mradi huo utahusisha ujenzi wa njia Kuu ya Reli yenye urefu wa kiliometa 249 na njia za michepuo zenye jumla ya urefu wa kiliometa 92 pia shughuli za awali za mradi huo zimeanza ambapo Mkandarasi aliwasili maeneo manne kwa ajili ya ujenzi wa kambi kuu za mradi.

" Katika Mkoa wa Mwanza Mkandarasi amewasilisha maombi ya maeneo mawili kwa ajili ya ujenzi wa kambi hizi katika Kijiji cha Feli Wilaya ya Misungwi na Kijiji cha Nkalalo Wilaya ya Kwimba " alieleza Bunzu .

Kwa upange wake Mwenyekiti wa kitongoji cha Feli Johari Hassan amesema ombi lao kubwa ni vijana wa maeneo hayo na jilani kupewa kipaumbele wakati ajira zitakapoanza kutolewa  kwani vijana wengi kwa sasa wapo mtaani hivyo wapewe kipaumbele na kusiwepo na ubaguzi.







Chanzo: ippmedia.com