Watanzania 350 wamenufaika na ajira za awali za ujenzi wa mradi wa Bomba la mafuta ghafi katika eneo litakalojengwa miundombinu ya kuhifadhia mafuta Chongoleani, mkoani Tanga.
Hayo yamesemwa Mratibu wa mradi wa Bomba la mafuta upande wa Tanzania, Asiad Mrutu wakati akitoa taarifa ya hatua zilizofikiwa katika mradi huo kwenye eneo la Chongoleani kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
Amesema kuwa kati ya hao Watanzania 150 wakazi wa eneo la mradi wameweza kunufaika moja kwa moja na ajira hizo, huku 250 wanatoka katika maeneo mengine ya Tanzania.
"Fursa za ajira zitaendelea kuongezeka kwa kadiri mradi unatakavyoweza kufikia hatua mbalimbali lengo ni mradi huo kuweza kuimarisha uchumi wa nchi lakini na mahusiano na nchi jirani,"amesema Mrutu.