Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watalii wazidi kumiminika Kilwa

Watalii Kilwa (600 X 326) Watalii wazidi kumiminika Kilwa

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meli ya kitalii kutoka Ufaransa ya Le Bouganiville ikiwa na watalii 146, imetia nanga Wilayani Kilwa tayari kwa watalii hao kujionea hifadhi ya urithi wa utamaduni wa dunia wa magofu kale yaliyoko Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, mkoani Lindi.

Akizungumza baada ya kuwapokea watalii hao, Mkuu wa Hifadhi hiyo ya Utamaduni na Malikale, Mercy Mbogela amesema meli hiyo ni ya sita kutia nanga Kilwa ndani ya mwezi huu wa Februari baada ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) kufanya maboresho katika hifadhi hiyo.

Maboresho ambayo sasa yanavuta watalii wengi kuja kujionea historia na utamaduni wa watu wa Afrika Mashariki yalihusisha, pamoja na mambo mengine, ujenzi wa jengo la mapumziko kwa wageni na ununuzi wa boti za kisasa zenye kioo cha kutazama vivutio vilivyopo baharini.

Baadhi ya vivutio vilivyopo Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ni magofu ya nyumba za kale ukiwemo msikiti wa kwanza mkubwa wa Afrika Mashariki uliojengwa karne 11. Pia kuna ngome ya Mreno pamoja na makaburi ya masultan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live