Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watalii wamiminika Kilwa

9d28e6f1c7e3710464a5336cbb117f5f Watalii wamiminika Kilwa

Mon, 27 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makundi ya watalii 120 kutoka mataifa mbalimbali duniani yakiwemo Marekani, Japan, Uingereza, Ujerumani na Switzerland wamewasili Tanzania na meli ya kisasa ya Le Bellot katika mji wa Kilwa Kisiwani kujionea magofu ya urithi wa dunia.

Watalii hao waliwasili jana na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Zainabu Kawawa akiambatana na ujumbe wa maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ambao ulioongozwa na Ofisa Utalii Mwandamizi ,Steven Madenge na wananchi wa Kilwa Kisiwani.

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Zainabu Kawawa amesema magofu ya Kilwa yanayosimamiwa na Tawa yameendelea kuipa heshima wilaya hiyo na Taifa ambayo kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu imewasili eneo hilo meli yenye kuwaleta watalii kutoka mataifa mbalimbali Duniani.

“Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu leo ( Desemba 26, 2022) tumepokea tena meli ya kitalii iliyowaleta watalii 120 kutembelea magofu haya, ambayo ni urithi wa dunia ambapo pamoja na mambo mengine wameshangazwa na upekee wa kisiwa hiki na vivutio vilivyomo ” amesema Zainabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live