Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watalii kutoka Israel walivyotua uwanja wa KIA

WhatsApp Image 2021 08 02 At 7.00.26 PM 660x400.jpeg Watalii wakiwasili uwanja wa KIA

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Watalii 150 kutoka nchini Israel limetua katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alfajiri kwa ajili ya kutembelea hifadhi za taifa ambapo watalii hao ni sehemu wataliii 500 wanaotarajia kuingia nchini Tanzania.

“Tumepokea kundi la kwanza la watalii 150 kutoka Israel ni Soko kubwa la kiutalii Duniani na sasa inaonekana wameitambua Tanzania, wote tushikamane tuhakikishe hawa wageni wetu wakija basi wakiondoka wakaitangaze vizuri nchi yetu”- RC Arusha

“Mheshimiwa Rais wetu anatia mkazo kwenye kufanya nchi yetu ifunguke zaidi, Uchumi wetu uwe wa kisasa zaidi na Utalii mnajua ni Sekta yenye mchango mkubwa katika Uchumi wetu”-RC Arusha.

Tanzania inatajwa kuwa moja ya nchi yenye vivutio vingi vya utalii huku mapema mwaka huu ripoti ya Tripadvisor iliitaja mbuga ya wanyama ya serengeti , Tarangire, na Mlima Kilimanjaro kama vivutio bora duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live