Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Hungary Katalin Novák leo July 18,2023 wameongea na Vyombo vya Habari Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema Rais Dkt. Samia kwenye hotuba yake ni kwamba mwaka 2022 Tanzania ilipokea Watalii 7188 kutoka Hungary.
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Hungary Katalin Novák leo July 18,2023 wameongea na Vyombo vya Habari Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo moja ya mambo aliyoyasema Rais Dkt. Samia kwenye hotuba yake ni kwamba mwaka 2022 Tanzania ilipokea Watalii 7188 kutoka Hungary. “Mwaka 2022, Tanzania ilipokea watalii 7188 kutoka Hungary, sio idadi kubwa lakini ndio idadi kubwa zaidi ya Watalii kutokea Hungary kurekodiwa na tunaamini kuwa baada ya ziara yako Watalii wengi zaidi watatembelea Nchi yetu na pia tunawakaribisha Wawekezaji kutoka Hungary kuja Tanzania kutafuta fursa za uwekezaji katika Sekta mbalimbali ikiwemo Utalii”