Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watalii 64 waingia nchini kwa kutumia reli ya Tazara

15062 Watalii+pic TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watalii 64 kutoka Ujerumani wamewasili leo Jumamosi Septemba Mosi, 2018 hapa nchini kwa kutumia Reli ya Tazara kwa lengo la kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii.

Watalii hao wametokea Afrika Kusini ambapo safari hiyo imewachukua siku 15 wakitumia treni ya kifahari ya Kampuni ya Rovos Rail ya nchini humo.

Wakiwa na furaha watalii hao walishuka kwenye treni hiyo na kuanza kusakata muziki uliokuwa ukipigwa na bendi ya polisi.

Wakizungumza na MCL Digital watalii hao wamesema wanavutiwa na hali ya hewa ya Tanzania na kubainisha shauku yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini.

“Nilikuwa nasikia Watanzania ni wakarimu nimefurahi kufika hapa hali ya hewa nzuri. Nategemea  itakuwa hivyo katika maeneo yote nitakayotembelea, safari yangu itaanzia Zanzibar,” amesema Anne Marie Derek

Meneja Mkuu wa Tazara Tanzania, Fuad Abdallah amesema ujio wa treni hiyo unazidi kuimarisha sekta ya utalii nchini na kuchangamsha uchumi wa shirika hilo.

“Ugeni huu ni mkubwa na una faida kubwa kwa Taifa,  kwanza ni treni ya kifahari inawaleta watu kutoka mataifa mbalimbali na vilevile inavyopita kwenye reli yetu Tazara tunalipwa hivyo tuna kila sababu ya kufurahia,” amesema 

Chanzo: mwananchi.co.tz