Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watalii 531 wafika Zanzibar kutoka Urusi

81e041d0ef74a37a1cdea1b8aae99478 Watalii 531 wafika Zanzibar kutoka Urusi

Mon, 2 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ZAIDI ya watalii 531 wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakitoka Urusi.

Idadi hiyo ni kubwa ya watalii kuwasili nchini kwa wakati mmoja baada ya kumalizika kwa janga la kusambaa kwa virusi vya corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19.

Kamisheni ya Utalii Zanzibar imeeleza kuwa, watalii 1,321 waliowasili Zanzibar katika kipindi cha siku nne za Uchaguzi Mkuu wakitoka nchi Ulaya ya mashariki ya Russia na Kazakhstan.

Katibu Mtendaji wa kamisheni hiyo Dk Abdalla Mohamed alisema watalii hao waliokuja kwa ndege ya ndege ya Shirika la Ndege la Azur la Russia ni dalili njema za ujio wa watalii baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kufungua milango kwa watalii baada ya kumalizika janga la corona.

“Tumepokea jumla ya watalii 531 wakitoka katika nchi ya Russia na kufanya jumla ya idadi ya watalii walioingia nchini katika kipindi cha siku nne za harakati za uchaguzi mkuu kufikia 1,321”alisema Mohamed.

Kamishna wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Khamis Mbetto alisema hiyo ni sehemu ya juhudi za kamisheni kufungua milango ya masoko ya utalii katika nchi za bara la Asia hadi mashariki ya mbali.

Alisema wanatarajia kupokea idadi kubwa zaidi ya watalii kutoka nchi za Skandnavia zikiwemo Norway na Sweden baada ya kufanya mawasiliano mazuri na ofisi za ubalozi zilizopo kwenye nchi hizo.

“Tunatarajia kupokea watalii wengi zaidi katika kipindi cha mwezi ujao kutoka nchi za Skandinavia hadi Ulaya ya mashariki ikiwemo nchi za Kazakhstan''alisema.

Wakala wa kampuni ya Enex ambayo ndiyo iliyoleta idadi kubwa ya watalii kutoka Russia Eray Atmis alisema wanatarajia kuleta watalii 1,000 kabla ya kumalizika kwa mwaka huu.

Alisema soko la utalii la Zanzibar katika nchi za Ulaya ya mashariki lipo juu na kwamba, Zanzibar inajiuza yenyewe kwa jina lake lililobeba historia kubwa.

Chanzo: habarileo.co.tz