Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kuitumia Taliri kufanya ufugaji wa kisasa

5d33959e803b561302c0874a52fada66 Watakiwa kuitumia Taliri kufanya ufugaji wa kisasa

Tue, 5 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAFUGAJI katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wametakiwa kutumia Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI), kujifunza juu ya ufugaji bora na wenye tija.

Imeelezwa kuwa ni vyema wafugaji wakajifunza kuwa na mifugo michache yenye tija kuliko kuwa na mifugo mingi isiyokuwa na tija wala kuwabadilisha kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wi?aya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri wakati akizungumza na wafugaji wa Kata ya Luhundwa.

Alisema kwamba katika ziara yake hiyo amegundua kuwa bado wananchi wengi wanafuga kizamani kwa kuwa na mifugo mingi isiyokuwa na tija na hiyo inatokana na kutotumia kituo cha utafiti wa mifugo cha Taliri kujipatia elimu ya ufugaji bora na wa kisasa.

"Inasikitisha kuona kituo chaTALIRI kinawafaidisha wafugaji kutoka nje ya Mpwapwa huku hapa wilayani bado wanafuga kienyeji, inasikitisha sana," alisema Shekimweri

Alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imejikita kuhakikisha wafugaji wanabadilika na kufuga kisasa ili waweze kunufaika kiuchumi kwa kuwa na mifugo michache yenye tija na manufaa.

"Unakuta zizi lina ng'ombe 400 ambao wamekonda na hawana ubora wakati angeweza kuwa na ng'ombe 100 wenye uzito mkubwa ukiangalia mifugo iliyopo Taliri inavutia kwa ukubwa na uzito. Sasa mifugo kama ya Taliri nataka kuiona kwa wananchi huko vijijini iwabadilishe kimaisha na kiuchumi," alisema Shekimweri

"Sasa niwaagize maofisa mifugo Kata zote kuwapitia wafugaji na kuwaangalia ufugaji wao na kuwapatia elimu ya ufugaji bora na wenye tija na pia muanzishe daftari la mifugo katika Kata zote ili kuweza kujua kila Kata ina mifugo kiasi gani na changamoto zinazo wakabili wafugaji," alisema mkuu huyo wa wilaya.

Chanzo: habarileo.co.tz