Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakiwa kuchangamkia fursa kilimo cha kahawa

Kahawa Pc Watakiwa kuchangamkia fursa kilimo cha kahawa

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, wametakiwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la kahawa, lengo likiwa kujiinua kiuchumi, kuongeza uzalishaji wa zao hilo pamoja na pato la taifa.

Akizungumza katika hafla ya ugawaji wa miche bora ya kahawa katika vitalu sita vilivyopo Kijiji cha Mwese Halmashauri ya Tanganyika mkoani Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu ametoa rai hiyo baada ya kuona idadi kubwa ya wakulima wa zao hilo la kahawa katika kijiji hicho ni wazee.

Amewataka vijana badala ya kucheza 'pool table' na kukaa vijiweni, walime zao la kahawa, kwani lina tija na ukanda huo una ardhi inayokubali kilimo cha mazao ya aina yoyote.

Naye Ofisa Maendeleo zao la kahawa Kanda ya Magharibi, Jasson Michael kutoka Bodi ya Kahawa Tanzania, amesema mpango mkakati wa bodi ya kahawa ni kuongeza uzalishaji wa zao hilo kutoka tani 82,000 za sasa hadi kufikia tani 300,000 kitaifa.

Amesema ili kufikia lengo hilo miche ya kahawa bora, zaidi ya 600,000 imepandwa katika Halmashauri ya Tanganyika kupitia bodi ya kahawa na ndio imegawiwa kwa wakulima wa kahawa maeno ya Lugonesi na mwese kwa ajili ya uzalishaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live