Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakaokiuka kanuni maadili ya manunuzi kukiona

Sheria Manunuziii Watakaokiuka kanuni maadili ya manunuzi kukiona

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma, wazabuni na wafanyabiashara watakaokiuka kanuni za maadili ya manunuzi ya umma

Akizindua rasmi Kanuni za Maadili kwa watumishi wa umma na wazabuni wanaoshiriki kufanya shughuli za ununuzi wa umma, Chande amesema lengo ni kuhakikisha kuwa asilimia 60 ya bajeti ya ununuzi wa umma inafanyika vizuri.

Amesema katika bajeti ya mwaka 2021/2022 ya ununuzi wa umma umechukua Sh20.48 trilioni sawa na asilimia 56 ya bajeti nzima ya nchi hivyo watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Emmanuel Tutuba amesema lengo la kanuni hizo ni kuhakikisha manunuzi ya umma ambayo yanachukua sehemu kubwa ya bajeti yanafanyika kwa uadilifu na kwa haki.

Amewataka wazabuni kuwasilisha zabuni kwa uadilifu ili kupata thamani ya fedha inayotarajiwa na kuleta tija na manufaa kwa wananchi.

Tutuba amesema bado taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi Nchini (PPRA) zinaonyesha kuwa kumekuwa na matukio ya ukiukwaji wa maadili na ndio maana wameandaa kanuni hizo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu (Sera za Ununuzi wa Umma) Dk Frederick Mwakibinga amesema awali kanuni zilikuwa zikiwahusu watumishi wa umma pekee lakini sasa zimeandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha watumishi na wazabuni wote wanazingatia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live