Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakaojiunga na DP World kuacha kazi TPA

Bandari Tanga Tangaaa Watakaojiunga na DP kuacha kazi TPA

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari (TPA) imesema kuwa imewapa watumishi wake nafasi ya kuchagua ama kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira na TPA na kuajiriwa na kampuni ya DP World ya Dubai.

TPA ilisema hayo katika taarifa yake ya ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za watumishi wake katika Bandari ya Dar es Salaam na ilisema kuwa Machi 20, ilitoa taarifa kwa watumishi wake juu ya mabadiliko ya uendeshaji wa bandari hiyo, gati namba sifuri (RoRo) hadi gati namba saba.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa TPA katika taarifa yake ya Machi 20, mwaka huu watumishi walielekezwa kuwa mabadiliko hayo yamesababishwa na mkataba wake na Kampuni ya DP World ya Dubai kwa miaka 30 kuanzia Oktoba 22, mwaka huu.

“Kutokana na mabadiliko hayo katika usimamizi na uendeshwaji wa maeneo tajwa, Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam walitakiwa kuchagua ama kubaki TPA au kusitisha mkataba wa ajira na TPA na kuajiriwa na DP World papo hapo,” ilifafanua taarifa hiyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live