Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakaoiwakilisha Serikali ya Tanzania katika kampuni ya Twiga hawa hapa

99886 Pic+mpango Watakaoiwakilisha Serikali ya Tanzania katika kampuni ya Twiga hawa hapa

Thu, 26 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Philip Mpango  amewateua wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali kwenye bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya madini ya Twiga.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Machi 22, 2020 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo, Benny Mwaipaja inaeleza kuwa wajumbe alioteuliwa ni Casmir Kyuki na Michael Kambi.

Uteuzi wa wajumbe hao watakaotumikia nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitatu unafuatia makubaliano mapya ya namna ya kuendesha kampuni hiyo kwa ubia yaliyofikiwa kati ya Serikali na kampuni ya Barrick Gold na kutiwa saini Januari 24 , 2020 jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya madini ya Twiga inasimamia migodi mitatu ya Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu ambapo Barrick Gold inamiliki asilimia 84 ya hisa na Serikali ya Tanzania asilimia 16.

Uteuzi wa wajumbe hao unaanza leo Jumapili Machi 22, 2020.

Chanzo: mwananchi.co.tz