Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watakao zembea kulipa kodi kuondolewa kwneye vitalu

ULEGA JUNI 2019 Watakao zembea kulipa kodi kuondolewa kwneye vitalu

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema kuwa mwekezaji yeyote atakayezembea kulipa kodi ya pango katika vitalu vya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) atatolewa ili apewe mwekezaji mwingine mwenye uwezo wa kuendeleza eneo hilo.

Ulega ametoa kauli hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa programu ya kopa ng’ombe lipa maziwa iliyofanyika wilayani Karagwe, mkoani Kagera Januari 23, 2023.

“Yeyote atakayezembea katika vitalu hivyo, halipi kodi, hafanyi uwekezaji wowote wa maana, anaacha mapori na vichaka, hatujui ana ng’ombe wangapi, anapeleka soko gani, tutamtoa tumuweke mtanzania mwingine atakayeweza kufanya kazi hiyo”, alisema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live