Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataka fidia kuipa serikali soko

83ffca0e461fc9f7af9fc5a30e89babb Wataka fidia kuipa serikali soko

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAFANYABIASHARA wa soko la Nakasero wameitaka serikali iwalipe fidia ya Sh bilioni 300 kama inataka kulichukua kuliendesha.

Wamesema hayo kutokana na azimio la Baraza la Mawaziri kutaka masoko yote ya umma jijini Kampala yamilikiwe na serikali ili kupunguza changamoto katika usimamizi.

Wafanyabiashara hao kupitia wakili wao, Paul Kenneth Kakande wamesema wana hati ya kumiliki eneo hilo kwa miaka 49 na kwamba serikali kuchukua eneo hilo kutawasababishia hasara kubwa.

Wafanyabiashara walikodisha eneo hilo kutoka Mamlaka ya Jiji la Kampala (KCCA) kwa Sh bilioni 2 wanatakiwa kulipa kodi ya ardhi ya Sh milioni 90 kila mwaka.

Kakande alisema serikali haikuangalia vizuri masuala ya kisheria yanayozunguka soko la Nakasero na badala yake imeagiza KCCA kuchukua kituo hicho mara moja.

Alisema ingawa sheria inaruhusu serikali kuchukua ardhi, lakini inapaswa kufanywa hivyo kisheria kwa kulipa fidia wenyeji ambao wana haki na ardhi husika.

"Wafanyabiashara wana mkataba ambao bado unaendelea na wana matarajio ya kufanya biashara kwenye ardhi hiyo na ndiyo sababu walichanga fdha kukodisha ardhi. Kwa hivyo kama unalihitaji eneo lazima ulipe fidia kulingana na matarajio yao ya kile wangeweza kupata katika miaka 49,”alisema.

Alisema soko la Nakasero haliko tu katika eneo muhimu la kipaumbele kufanya biashara, lakini lina wafanyabiashara zaidi ya 5,000 wanaofanya biashara kwa lengo la kupata faida.

Chanzo: www.habarileo.co.tz