Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watafiti waja na chanzo samaki kuvilia damu

Samaki Pic Watafiti waja na chanzo samaki kuvilia damu

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TATIZO la ugonjwa wa kuvilia damu na vidonda kwa samaki wa kufugwa aina ya sato, sasa limepatiwa ufumbuzi baada ya kupatikana kwa chanjo.

Hilo limebainika wakati timu kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), ilipofanya ziara katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kilichopo Morogoro kujionea namna fedha za serikali kupitia tume hiyo zinavyotatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Mtafiti wa chanjo hiyo kutoka SUA, Dk Alexander Mzula anasema chanjo hiyo imeshawanufaisha wakulima 96 kwenye Mikoa ya Ruvuma, Mwanza, na Arusha na inategemewa kunufaisha wafugaji wa sato kwenye mabwawa na vizimba zaidi ya 10,000.

“Chanjo hii itaongeza udhibiti wa ugonjwa huu ukilinganisha na utaratibu wa utunzaji wa mabwawa bila kutumia kinga yoyote kwa samaki sato,” anasema.

Anaeleza kuwa ametafiti chanjo hiyo kwa hatua ya pili kwa ufadhili wa serikali kupitia Costech na ulilenga kujiridhisha na ufanisi wa chanjo hiyo ya kuzuia ugonjwa usababishwao na bakteria aina ya aeromonas hydrophila.

Ugonjwa huo wa kuvilia damu na vidonda ndio umekua tatizo kubwa ulimwenguni kote ambao unaweza kuua mpaka asilimia 100 ya samaki bwawani.

“Hapa kwetu Tanzania ugonjwa huu umeshajitokeza kwenye mikoa mbalimbali kama Ruvuma, Mbeya, Kilimanjaro, Iringa na Mwanza,” anasema.

Kuhusu samaki wa kufugwa Dk Mzula anasema huugua sana magonjwa mbalimbali ukilinganisha na samaki wasiofugwa.

Sababu kubwa ni uangalizi mdogo wa samaki hao kwenye mabwawa ikiwa ni pamoja na kujazana wengi ikilinganishwa na ukubwa wa bwawa, kutosafisha bwawa na kubadilisha maji, hali ambayo huwaweka samaki katika shinikizo la kupata magonjwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live