Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wataalamu wa ujenzi Tanzania wamwangukia Rais Magufuli

74203 Wahandisi+pic

Wed, 4 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wataalamu wa ujenzi Tanzania wamemwomba Rais John Magufuli wa nchi hiyo kutatua changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa hilo.

Wataalamu hao ni Bodi ya usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) wamesema hayo leo Jumatano Septemba 4, 2019 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mashauriano baina yao na Rais Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa CRB, Consolata Ngwimba ameanza kwa kusema wamekuwa wakichukua hatua kwa wanachama wao ambao wanabainika kukiuka taratibu.

“Wale ambao watakiuka maadili ikiwamo rushwa, watachukuliwa hatua kali za kisheria, nichukue fursa hii kuwaasa wataalamu wenzangu kutelekeza wajibu wao ipasavyo,” amesema Ngwimba

Akibainisha changamoto, Ngwimba ameomba Serikali ya Tanzania ijenge mazingira wezeshi ya kisheria ili kuhakikisha ushiriki wa wazawa kiusawa katika miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Tanzania.

Amesema kwa sasa ili waweze kushirikisha wataalamu wa ndani ni vile mtu anajisikia na si lazima kutupatia.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

“Tunajitahidi kwa uwezo wetu kama bodi ya CRB, tumeunganisha unganisha wakandarasi na kuwapeleka kule mfano kwenye umeme wa Rufiji, kwa sababu si sheria tunaomba omba na hata fedha wanayopewa wanaishia kukata tamaa. Tunaiomba sana serikali, hili liweke vizuri,” amesema

Mwenyekiti huyo amesema changamoto nyingine ni masharti yasiyo rafiki yanayotolewa katika zabuni zetu.

“Kwa mfano wakati sheria inatoa uhuru mwajili kuruhusu dhamana ya bima au benki lakini watendaji wengi wa Serikali wamekuwa wakilazimisha kutoa bima za benki peke yake na hii imekuwa ngumu kwelikweli.”

“Sheria inasema bima au benki, tunaomba sana mheshimiwa Rais (Magufuli) na tunaomba kwa kupitia kwako, wale wanaoshughulika kutoa miradi hii waiangalie sheria na kutumia vilivyo,” amesema huku akishangiliwa na washiriki wa mkutano huo

Ameongeza, “kwa sababu sasa hivi bima zetu zinafanya vizuri, hata maisha yetu tunakabidhi kwenye bima, tunawaomba kweli. Hili likiwekwa vizuri litasaidia wakandarasi wetu kushiriki vizuri.”

Awali, Mwenyekiti wa ERB, Profesa Ninatubu Lema amesema ujasiri na uthubutu unaofanywa na Rais Magufuli wa kuwa na malengo makubwa ni somo kubwa sana, Watanzania na hasa wahandisi ni fursa kubwa.

“Tunahitaji kujiamini sana na hii ni muhimu sana ili kuwa na viwanda endelevu na viwanda endelevu ni vile vya wazalendo. Tunaposonga mbele lazima tujikite katika kuelekeza nguvu huko.”

Amesema bodi ya ERB inategemea kuwa na kituo cha wahandisi jijini Dodoma kitakachofanya kazi ya kuhamasisha uzalendo katika kujenga viwanda na baada ya miaka kumi na zaidi viwanda viwe vya wazalendo.

“Wahandisi na watalaam wa sekta ya ujenzi, tuendelee kutumika kwa weledi na kufanya hivyo tutaijengea Serikali imani, tulikotoka ni tofauti tulipo na tunapokwenda.”

“Tunaomba uendelee (Rais Magufuli) kutuamini na kututumia kadri unavyoweza, hatuwezi kushindwa kutoa huduma,” amesema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya AQRB, Dk Luligija Bulemule ametoa wito kwa kampuni za wazawa kushirikiana kwani, “kampuni zetu ni moja moja au mbili mbili na kiuhalisia si rahisi kushindana (hivyo) tuweze kuwa na ushirikiano mkubwa zaidi ya kuziwezesha kampuni zetu kukua na kushindana na kampuni zingine.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz