Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasindikaji wa mpunga walilia masoko ya kikand

0d3b8978cf2bc0ac7fc69a70753cf31d Wasindikaji wa mpunga walilia masoko ya kikand

Fri, 22 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WASINDIKAJI wa zao la mpunga nchini wamelilia soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ili waweze kukuza uchumi wao.

Wamesema kwa sasa wamekosa soko na kujikuta wakiuza bidhaa zao kwa bei ndogo na kwa kiwango ambacho hakiwawezeshi kukuza uchumi wao.

Wamesema kumekuwapo na ongezeko la uzalishaji wa mchele kutoka tani milioni 1.2 na kufikia tani milioni 1.8 nchini lakini changamoto kubwa ni ukosefu wa masoko.

Wasindikaji hao walitoa kilio hicho jana kwenye mafunzo ya usindikaji wa zao la mpunga yaliyoandaliwa na Baraza la Mchele Tanzania (RCT) kwa kushirikiana na Repoa kupitia mradi wa Tradecom 11 na kufadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (EU).

Msindikaji, Victor Muzo alisema mchele upo mwingi ila masoko hakuna.

(Kama wangekuja wafanyabiashara kutoka nje kama Kenya na Uganda kama ilivyokuwa zamani tungeweza kunufaika,” alisema.

Msindikaji mwingine, Andrew Siria alisema hivi sasa wanategemea wateja wa ndani na hakuna bei elekezi kila mmoja anauza anavyotaka.

Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo, Annamringi Macha alisema kuwapata wanunuzi inatakiwa wakulima wajiunge na Mtandao wa Ununuaji Mazao Tanzania (TMX) kwani huko wanunuaji wataingia moja kwa moja kujua bei wanayoitaka na kununua bila usumbufu.

"Serikali haijazuia wanunuzi kutoka nje bali upo utaratibu unatakiwa kufuatwa kiusalama, hivi sasa milango itafunguliwa ili wakulima waweze kunufaika, siwezi kulizungumzia hili hapa, bado lipo kwenye utaratibu natumaini mtajulishwa hilo halina shaka," alisema Ndanya.

Mkurugenzi Mtendaji wa RCT, Winnie Bashagi alisema asilimia 80 ya mpunga nchini hulimwa na wakulima wadogo kati ya hekta 0.2 hadi mbili na hutegemewa na wafanyabiashara wa mchele.

Alisema Baraza la Mchele limetoa mafunzo kwa wasindikaji 100 ili kuwajengea uwezo waweze kuzalisha mchele bora wenye viwango vinavyokidhi ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi.

Chanzo: habarileo.co.tz