Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washiriki Jukwaa la Fikira wapigia chapuo kilimo

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wadau wanaoshiriki Jukwaa la Fikra la Mwananchi, wamepigia chapuo suala la kilimo katika kufikia Tanzania ya Viwanda.

Wakichangia mada ya utumiaji wa rasilimali zilizopo katika kufikia uchumi huo lililobeba mada kuu ya kuelekea uchumi wa viwanda tujadili fursa, changamoto na ufumbuzi, leo usiku Oktoba 4, 2018  wamesema bila kilimo kupewa kipaumbele kampeni hiyo haitafanikiwa.

Filbert Philipo, kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), amesema ifike mahali wanaomiliki viwanda vya juisi  kwenda vijijini kuzungumza na wakulima wa matunda namna ya kufanya nao biashara, badala ya kuwaachia madalali kufanya kazi hiyo.

Mshiriki mwingine, Dastan Shega amesema hata nchi ya Marekani ilipofika kwa maendeleo, ilianza kuwekeza katika kilimo jambo ambalo hata Tanzania inaweza kwani imejaliwa rasilimali nyingi kufanikisha hilo ikiwamo maji na ardhi yenye rutuba.

Alexandra Njombe ambaye ni mbia wa kampuni ya  KPMG, amesema bila Watanzania kuwa tayari kubadilika uchumi wa viwanda itakuwa ni ndoto.

"Mafuta, gesi vyote vinahitaji wataalamu katika masuala ya uchumi na fedha, hivyo kuna kila sababu ya Watanzania kuwa tayari kubadililika," amesema.

Mfanyabiashara wa Bandari Kavu, Martha Egina amesema uchumi wa viwanda unapaswa kujulikana kuanzia kwa watoto wakiwa shule za msingi, kwani wengi wao wamesikia wakiwa vyuoni jambo linalofanya kuwa ngumu kwao kuelewa na kutekeleza.

Chanzo: mwananchi.co.tz