Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Washawishiwa kujikita kwenye kilimo cha pilipili

8a3b1189bdcef0ad81440ee2fd7dab58 Washawishiwa kujikita kwenye kilimo cha pilipili

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAKULIMA wa Kaskazini na maeneo ya ukanda wa Pwani wameshauriwa kujikita katika kilimo cha pilipili, mboga na matunda ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Arusha na kueleza mikakati ya Asasi Kilele inayojishughulisha na masuala ya maua, mbogamboga, matuda, mimea itokanayo na mizizi na viungo (TAHA) sanjari

na utendaji kazi, Meneja Mkuu wa Maendeleo, Anthony Chamanga, alisema fursa ya zao la kilimo cha pilipili zipo nyingi na uhitaji wake ni mkubwa kwa soko la nje.

"Kilimo cha pilipili za aina mbalimbali ni fursa kwa wakulima, hivyo natoa rai kwa wakulima kulima zao hilo kwani baadhi ya nchi za nje wanazihitaji kwa wingi," alisema Chamanga.

Alisema licha ya kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa Corona mwaka jana,lakini sekta ya kilimo ilikuwa na fursa ya masoko ya kikanda na kimataifa na bidhaa mbalimbali ziliweza kusafirishwa kwa ndege kupitia

uwanja wa KIA.

Naye Meneja wa Sera na Utetezi, Kelvin Remen alisema TAHA hivi sasa imejikita kuhakikisha wakulima wananufaika na mazao wanayozalisha.

Chanzo: habarileo.co.tz