Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wasafiri nchini kunufaika na mfumo malipo ya kidigitali

Thu, 7 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WASAFIRI nchini wataanza kunufaika na mfumo wa malipo kwa njia ya kidigitali.

Mfumo huo mpya wa malipo kwa njia ya kidigitali kwa wasafiri nchini (EYWA), ulizinduliwa juzi na Kampuni ya MasterCard kwa kushirikiana na kampuni ya utoaji huduma za usafiri - EYWA na Benki ya NMB.

Huduma hiyo ambayo itakuwa ndani ya kadi maalumu za kielektroniki pia watumiaji wa simu za mkononi wataweza kupata taarifa huku watumiaji wa simu rununu (smartphone) watakuwa na uwezo wa kupakua programu maalumu kupata maelezo ya huduma hiyo.

Uwepo wa progamu hiyo itakuwa suluhisho la changamoto za huduma za usafirishaji nchini kwa kupunguza matumizi ya mfumo wa malipo ya fedha taslimu na kuja na mfumo wa malipo kwa njia ya kidijitali kwa mamilioni ya abiria nchini.

Kwa uwezeshaji wa Mastercard QR, EYWA na Benki ya NMB, wasafiri wanaweza kupunguza mawasiliano ana kwa ana na kupata huduma za usafiri kwa njia salama. Huduma hii inawawezesha wasafiri kuacha kupanga foleni za ununuzi wa tiketi; kurudi kuangalia muda wa safari.

Kwa kupitia simu za mkononi na kadi maalumu, wasafiri wataweza kukata tiketi kwa njia ya kidijitali na kupunguza muda wa huduma husika.

Watoa huduma za usafiri au wamiliki wa mabasi kwa upande mwingine wataweza kukagua orodha ya abiria waliofika katika kila kituo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa EYWA, Toffène Kama, alisema: "Tumejitolea kutoa huduma bora za usafirishaji watu wengi kupatikana kwa urahisi na kuwezesha mamilioni ya Waafrika kusafiri salama kila siku, kwa gharama wanazoweza kumudu.

Wakati dunia inakabiliwa na janga la COVID-19, tunafurahi kuzindua huduma hii ambayo itawawezesha wasafiri Tanzania kusafiri huku wakiwa salama kwa kupunguza huduma zinazowalazimu kuonana ana kwa ana kila mara.”

“Kupitia Mastercard QR na teknolojia yetu ya kipekee, huduma hii inarahisishaji ukusanyaji wa nauli kutoka maeneo mengi kwa njia mbalimbali katika mfumo mmoja. Ni mfumo rahisi, salama usio na shida kwa madereva na abiria wote,” alisema na kuongeza:

“Tunapongeza juhudi za Chama cha Wasafirishaji jijini Dar es Salaam (UWADAR) na juhudi zao nyingine katika kuhakikisha mtandao wao wa madereva unatumia mfumo huu kutoa huduma bora kwa wateja wao.”

Mkuu wa Biashara kutoka MasterCard Ukanda wa Afrika Mashariki, Mastercard, Adam Jones, alisema: "Wakati watu wakisafiri zaidi kuelekea katika maeneo ya mijini kwa lengo la kufanya kazi au kupata burudani, mamlaka za miji zinatafuta mfumo rahisi wa pamoja wa usafiri wa umma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, alisema: "Tumejitolea kukuza sekta ya usafirishaji Tanzania na kufanya kazi na washirika kama EYWA na Mastercard kuanzisha mfumo wa malipo ya kidijitali ambao mbali na kupunguza matumizi ya fedha taslimu pia utakuwa na faida kwa wasafiri au abiria na uchumi kwa ujumla.

“Utaratibu huu wa malipo ni sehemu muhimu ya mikakati ya NMB kutoa mfumo jumuishi wa kifedha kwa watoaji huduma za usafiri na sekta nzima kwa ujumla.

“Kwa kushirikiana na Mastercard QR, tunatoa njia bora kwa wasafiri kupokea malipo kutoka kwa watoaji wa huduma za usafiri na wateja wa benki za kibiashara ambazo zimeunganishwa na huduma za Mastercard QR,” alisema Zaipuna.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live