Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapewa mbinu waweze kukopesheka

Fedhapic Wapewa mbinu waweze kukopesheka

Sun, 17 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKULIMA wa mazao Mchanganyiko wilayani Momba, mkoani Songwe wametakiwa kuunda vyama vya Ushirika (AMCOS), ili waweze kukopesheka na kuwa na uhakika wa soko la mazao yao.

Hayo yamesemwa na mtalaam wa uendelezaji Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB ), Marco Ndonde katika ziara ya watalaam wa Wizara ya Kilimo wakiambatana na Mbunge wa Jimbo la Momba, Condester Sichalwe kutoa elimu ya kilimo bora kulingana na mabadiliko ya tabianchi katika wilaya hiyo.

Amesema Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, kazi yao kubwa ni kununua mazao mchanganyiko kwa wakulima na kuyachakata, ambapo wana viwanda mbalimbali vikiwemo vya kusaga unga wa mahindi, mihogo, ngano na siagi.

Amesema ili kuendesha viwanda vyao wanahitaji mazao mengi kutoka kwa wakulima, ambapo wanaingia mikataba na taasisi , AMCOS na mkulima mmoja mmoja ili kumsaidia kupata mikopo ya kumsaidia kuzalisha kwa wingi .

Amesema wanapenda zaidi kufanya kazi na AMCOS kwa sababu ni rahisi kupata mazao mengi na kupanga bei yenye tija, ambayo inamuinua mkulima ambalo ndio lengo kubwa la bodi hiyo.

“Wakulima wa kiwa kwenye vikundi ni rahisi kuwasaidia kwa sababu hata mwenye mavuno kidogo ananufaika kupitia ushirika wao wa kukusanya mazao kwa pamoja na kuyauza kwa bei nzuri waliopanga wao,” amesema Ndonde.

Naye mtafiti kutoka Kituo cha utafiti (TARI) Naliendele, Mtwara Zabron Ngamba amesema wakulima wakiwa kwenye ushirika ni rahisi kupanga bei ya mazao yao na rahisi kumwita mteja kutoka ha nje ya nchi kununua mazao yao.

Amesema pia kwenye vikundi wakulima wanakuwa na sauti ya pamoja, ambapo ni rahis kuwashirikisha viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya wilaya mpaka Taifa kushauriana kuhusu soko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live