Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapangaji TBA wasaini mkataba kulipa bil 1.6

874ffb9d3f38a5aaca20629916e51523 Wapangaji TBA wasaini mkataba kulipa bil 1.6

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAPANGAJI 298 wanaoishi kwenye nyumba za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwenye eneo la Wazo Hill, Dar es Salaam wamesani mkataba wa miezi mitano unaowataka walipe malimbikizo ya madeni ya nyuma na kodi ya sasa ifikapo Juni mwaka huu.

Mwenyekiti wa kamati ya wadaiwa sugu wa TBA, Gilbert Mwasambo, alilieleza HabariLEO jana kuwa mkataba huo umesainiwa baada ya operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu Februari 3 mwaka huu.

Alisema siku moja baada ya operesheni hiyo, wadaiwa hao waliomba kuzungumza na TBA kutafuta suluhu na kuona namna ya kulipa madeni hayo kwa kuwa kuwafukuza ni aibu kwao.

“Tuliendesha operesheni ya kuwaondoa wadaiwa sugu 220 kwenye nyumba za Wazo, tulifanya hivyo baada ya wao kukaidi kulipa kodi ya pango kwa muda mrefu na kusababisha madeni ya shilingi bilioni 1.6, sasa wakati tumeanza operesheni hiyo walituomba tutafute suluhu kwa njia ya mazungumzo na tukakubali na wateja 298 wameingia nasi mkataba mpya na tayari wameshaanza kulipa madeni yao’’alisema Mwasambo.

Alisema wapangaji walianza kulipa malimbikizo ya madeni kuanzia Februari 8 mwaka huu na wanalipa kodi kulingana na hadhi ya nyumba baada ya kupewa namba ya malipo.

Alisema TBA eneo la Wazo Hill ina jumla ya nyumba 450, na kwamba, wapangaji 230 wamelipa madeni yao na 220 walikuwa wamekaidi lakini sasa wamesaini mkataba mpya na kukubali kuanza kulipa madeni.

Kwa mujibu wa Mwasambo nyumba za TBA Wazo Hill zipo katika hadhi tofauti kuanzia za kodi ya 30,000 hadi 350,000 kwa mwezi.

Alisema, baada ya Dar es Salaam operesheni hiyo inahamia Pwani na Morogoro ambako kuna deni la shilingi milioni 124.

Desemba mwaka jana, Mtendaji Mkuu wa TBA, Daud Kandoro, wakala unazidai taasisi 17 na wapangaji wengine 432 jumla ya sh bilioni 7.3 na kwamba, taasisi za serikali pekee zinadaiwa sh bilioni 4.18

Chanzo: habarileo.co.tz