Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania, inesema haitasita kumfutia leseni mfanyabiashara yoyote wa mbolea atakayepandisha bei ya mbolea kiholela na kupelekea shughuli za wakulima kukwama kutokana na bei hizo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamkala hiyo, Dkt. Stephan Ngailo wakati akizungumza na wadau wa mbolea ambapo amesema katika tathmini waliyoifanya mwezi Februari na Machi mwaka huu, imeonyesha uwepo wa mabadiliko makubwa ya bei za mbolea inayozidi asilimia 40 hadi kufikia asilimia 50.
Dkt. Ngailo amesema, mabadiliko hayo yamepelekea athari kubwa kwa wakulima hasa katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, kwa kuwepo na mfumuko mkubwa wa bei za mbolea usio wa kawaida, ambao haukutarajiwa kuwepo, kwakuwa hakuna taarifa za kuwasili kwa shehena mpya ya mbolea, ambayo inaweza kusabaisha mfumuko wabei hiyo.
Hata hivyo, Dkt. Ngailo ametumia kikao hicho kuwataka wafanyabiashara wa mbolea nchiniz kutumia uhuru wa kupanga bei waliopewa na mamlaka hiyo, ili kupunguza gharama za kilimo kama ilinavyotarajiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.