Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanunuzi wa kahawa kupelekwa ghalani

11350 Kahawa+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Missenyi. Serikali imesema wafanyabiashara kutoka nchi jirani wanaotaka kununua kahawa ya wakulima watapelekwa kwenye maghala ya vyama vya ushirika kama watakuwa na bei tofauti na inayotolewa.

Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba alitoa kauli hiyo baada ya kikao cha pamoja na Waziri wa Ushirika na Biashara wa Uganda, Ngobi Frederick ambacho pia kilihudhuriwa na Charles Mwijage ambaye ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

“Tumemuomba Waziri (Ngobi) alete wafanyabiashara waliotayari kutoa bei nzuri, kuliko sisi tutakayotoa; aje tutampeleka kwenye maghala yetu,” alisema Tizeba.

Katika mkutano huo, Waziri Mwijage aliahidi kuwa wizara yake itaendelea kurahisisha mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja huduma zote za vibali kupatikana eneo la mpakani. (Phinias Bashaya)

Chanzo: mwananchi.co.tz