Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanufaika mafunzo uongezaji thamani madini

Madini Pic Data Wanufaika mafunzo uongezaji thamani madini

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana 349 waliohitimu mafunzo ya fani mbalimbali za uongezaji thamani madini kutoka Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), wamepata fursa za ajira ikiwemo kujiajiri katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo Machi 20, 2024 katika ofisi za kituo hicho jijini Arusha na Kaimu Mratibu wa TGC, Jumanne Shimba katika kikao kazi na waandishi wa habari ambao wapo kwenye ziara ya kutembelea miradi ya kituo hicho.

"Vijana wengi ambao wamehitimu katika kituo hiki wamepata nafasi ya kuajiriwa na kujiajiri ikiwemo katika kampuni zinazofanya shughuli za uongezaji thamani madini kutokana na kuwa na ujuzi wa kiwango cha juu," amesema Shimba.

Amesema, idadi hiyo ya wahitimu ni tangu kituo hicho ambacho kina usajili wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kianze kutoa mafunzo mwaka 2015.

Shimba amesema, kituo hicho kinatoa mafunzo ya muda mfupi katika fani za ukataji na ung’arishaji wa madini ya vito, fani ya usonara, fani ya uchongaji wa vinyago vya vito, utambuzi wa madini ya vito na utengenezaji wa bidhaa za mapambo na urembo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live