Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanawake watajwa kuteka soko la uvuvi Afrika

Uvuvi Tanzaniaaaa Wanawake watajwa kuteka soko la uvuvi Afrika

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wachakataji na wafanyabiashara wa mazao ya uvuvi barani Afrika wametajwa kuwa na mchango mkubwa katika Sekta ya Uvuvi hususan katika uchatakaji na kilimo cha mwani.

Afisa Uvuvi Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Jovice Mkuchu amebainisha hayo Machi 21, 2024 jijini Dar es salaam wakati akifungua kikao cha mtandao wa wanawake barani Afrika wanaochakata mazao ya uvuvi kilicholenga kukuza uelewa wa uongozi katika nchi zao.

Aidha Bi. Mkuchu amesema, serikali inatambua umuhimu wa wanawake katika kuwezesha na kuendeleza Sekta ya Uvuvi barani Afrika, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akiwezesha na kuinua wanawake kwenye kilimo cha mwani na shughuli za uvuvi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wanawake Afrika Wanaojishughulisha na Uchakataji na Biashara ya Samaki (AWFISHNET) wenye makao makuu nchini Tanzania Bi. Editrudith Lukanga, amebainisha kuwa mtandao huo una wanawake ambao ni viongozi wa mtandao kutoka nchi mbalimbali takriban 44.

Bi. Lukanga amesema kuwa mtandao huo ulianzishwa Mwaka 2017 kwa msaada wa Umoja wa Afrika (AU) kupitia Shirika la Umoja wa Afrika la Rasilimali za Wanyama (AU-IBAR), ambapo katika kikao hiki kinachofanyika nchini moja ya malengo makuu ni kutafuta suluhu ya changamoto zinazowakabili wanawake katika Sekta ya Uvuvi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live